Alichokizungumza kapteni Komba kuhusu Mzee Warioba na Kinana…

No comments
image-06-11-14-04-17-10
Mbunge wa Mbinga Magharibi John Komba, leo Novemba 6 katika kikao cha Bunge amezungumzia mambo mawili ;-
1- Kuhusu kauli ya Mbunge Peter Msigwa juu ya Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana; “..kwa kuanza kwanza ni.. sikupenda sana kwa hotuba aliyoitoa mwenzetu Msigwa jana kuhusu katibu wetu mkuu Kinana wa CCM.. nataka nimuhakikishie Msigwa.. kati ya makatibu wakuu tuliowapata katika Chama cha Mapinduzi..waliokifanyia vizuri chama chetu cha mapinduzi… Kinana ni miongoni mwao na ndio tishio la upinzani kwa sasa hivi.. Kwa hiyo kumuingiza Kinana pale kumletea maneno ambayo hajayasema.. ni kiwewe tuu cha buree cha bure.. Kinana yupo pale kuwaondoeni nyie mnaosema mtachukua nchi…”—Komba
Komba2- Kuhusu alichofanyiwa Jaji Warioba; “.. Pili nitoe pole kwa mzee Warioba.. juzi yale yaliyompata pale siyo jambo jema.. na yeye anasema kwamba hayajawahi kuona tangu uhuru.. lakini angesikia ushauri wangu wakati ule wa Bunge la Katiba haya yasingetokea.. akae tuu pembeni .. aache mjadala wao uendelee kama kawaida na utaratibu uende kama kawaida yeye alimaliza kazi yake.. wengine wafanye kazi yao na katiba hii mwisho ipatikane nzuri.. ukiingilia ingilia hayo ndiyo yatakayokupata.. mzee pumzika tuu…”– Komba
Ukitaka kuisikiliza sauti ya Komba akizungumzia hayo leo Novemba 6 kwenye kikao cha Bunge, iko hapa bongyeza play

No comments :

Post a Comment