Inabidi ujue kabisa kwamba ukiingia Mlimani City na gari lako utakutana na hii
Mlimani City ni Shopping Mall ambayo ni maarufu kuliko zote za Tanzania kwa sasa, ni sehemu ambayo ina mkusanyiko mkubwa wa maduka na migahawa mbalimbali ambayo kwa miaka ya karibuni imesaidia kuleta mapinduzi ya sehemu za kufanyia shopping Tanzania.Na kwa miaka yote kumekua na utaratibu wa kawaida kwamba ukiingia na gari lako Mlimani City unapewa tu kadi ambayo unatakiwa kuiacha kwenye geiti wakati ukitoka na hautoulizwa kitu kingine hata ukilipaki gari lako kuanzia asubuhi mpaka jioni ila sasa hivi utaratibu umebadilika.
Yeyote anaeingia na gari ni lazima alilipie Parking ambayo inalipwa kutokana na muda uliopaki, ukipaki ndani ya dakika 60 hautochajiwa chochote ila dakika 60 zikizidi mpaka dakika 120 utalipia shilingi 500.
Kwenye dakika 120 (saa mbili) mpaka dakika 180 (saa tatu) utalilipia gari lako shilingi elfu moja wakati kwa saa tatu mpaka nne utalipia shilingi elfu moja mia tano na ukizidisha na kufikia saa tano itaongezeka shilingi mia tano kwa saa moja.
Wakati wa kutoka Mlimani City ni lazima ulipie parking kabla ya kutoka na gari lako, utakwenda kwenye vituo maalum na kuingiza kadi yako pamoja na kiwango unachodaiwa kama inavyoonekana hapa chini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment