Msanii wa filamu Bongo, Yusuf Mlela. |
MSANII
anayefanya vizuri katika filamu Bongo, Yusuf Mlela ambaye amekuwa
akidaiwa kutumia madawa ya kulevya maarufu kama unga, amesema utofauti
wa muonekano wake kwa sasa siyo kwa sababu ya uteja, bali inatokana na
umri wake kusogea.
“Unajua mtu
unavyozidi kukua na muonekano nao unabadilika, lakini itafikia kipindi
nitakuwa sawa tu hivyo naomba mashabiki wangu waelewe kwamba mimi siyo
teja na sijawahi kutumia ‘unga’ hizo ni habari za kizushi tu,”alisema
Mlela.
Hivi karibuni
Mlela alitupia picha kwenye mtandao wa Instagram ambapo wadau mbalimbali
walionekana kushangazwa na muonekano wake na kumfananisha na mateja.
No comments :
Post a Comment