Davido aondoka ukumbini baada ya Dj kupiga wimbo alioshirikishwa na Diamond "Number One Remix"

No comments

Baada ya kufanya show  Freedom City Mall nchini Uganda iliyokuwa na mafanikio makubwa weekend iliyopita nchini Uganda, Davido aliombwa kuhudhuria Laftaz iliyopo Centenary Park siku ya jumatatu usiku kwa ajili ya usiku wao wanaouita "Drunken Monday", usiku ambao unajuisha members wa team no sleep. 

Dili hilo lilisimamiwa na Pallaso ambae amefanya collable na Davido na muimbaji huyo alitokea akiwa na Davido ambae alikuwa amevaa jezi ya Cranes ya Uganda.

Kila kitu kilienda sawa, alipiga picha na mashabiki zake mpaka pale Dj wa sehem hiyo alipopiga wimbo wa Diamond  "Number One Rmx" aliomshirikisha Davido,
Davido alibadilika na kuondoka sehem hiyo huku akitoa maneno machafu. Licha ya kubembelezwa na meneja wa Hangout lakini Davido hakutaka kusikia chochote na kuondoka haraka kuelekea katika hoteli aliyofikia.

Mtandao wa matookerepublic umeripoti kuwa Davido ameuga na kuwa adui wa Diamod baada ya tuzo za Channel O Davido alipoondoka mikono  mitupu na Diamond kubeba tuzo 3. Davido amehisi kudharauliwa kwasababu Diamond kashinda tuzo kwa original version ya Number one huku Davido akihisi kuwa remix ya wimbo huo ndio umeufanya kuwa maarufu 

No comments :

Post a Comment